Viongozi watatu waitwa kuhojiwa kuhusu-NONDO.

In Kitaifa
Viongozi watatu wa nafasi za juu katika Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) wameitikia wito wa kufika kwa mpelelezi wa makosa ya Jinai (DCI) Jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa lengo la kuhojiwa kutokana na tukio la Abdul Nondo.
Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Afisa Habari- TSNP, Hellen Sisya baada ya kupita siku moja tokea Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuwataka viongozi hao kufika katika ofisi za DCI.
“Tumepokea taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inatofautiana kabisa na ile ya Iringa juu ya kuonekana kwake. Hata hivyo, kabla ya taarifa ya uchunguzi kulitanguliwa na matamko ya viongozi wa juu waliodai kuwa Abdul Nondo alijiteka mwenyewe jambo ambalo kwa vyevyote lingeathiri uchunguzi wa jeshi la polisi”, amesema Hellen.
Pamoja na hayo, Hellen ameendelea kwa kusema “pamoja na mapungufu yote tunaamini Nondo atatendewa haki atakapofikishwa mahakamani”.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu