Wabunge wa mkoa wa Dare s Salamu kupitia kwa mbunge wa
Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima,wametoa salamu za
pole kufuatia msiba wa mbunge wa jimbo la Kigamboni Dkt
Faustine Ndugulile.
Salamu hizo zimetolewa na mbunge Gwajima katika viwanja wa
Karimjee lilipokuwa likifanyika zoezi la watu mbali mbali
kuuaga mwili wa Dkt Ndugulile.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee
aliwakisha kambi ya wachache Bungeni,ametoa salamu za pole
akieleza mambo kadhaa,na kuongeza kuwa Dkt Ndugulile
alikuwa mtiifu na mkweli jambo ambalo lilimsababishia kupata
ajali za kisiasa enzi ya uhai wake.



