Wema Sepetu Amkata ngebe Harmo Rapper baada ya kusema atamuoa

In Burudani

Unajua Hii kitu inaitwa KIKI ni nzuri ukiitumia vizuri lakini ni mbaya pia ukiitumia Kupitiliza au ukitumia Kiki isiyo na mashiko.

Kuna Msanii Tanzania kwa sasa ambaye watu wengi wasema amekuwa Msanii wa KIKI, Msanii huyo anaitwa Harmo Rapper.

Pamoja na Kiki zote alizojaribu kutembelea ikiwa kutumia Majina ya Mastaa mbali mbali hata kwa kashfa ili kujikuza nayeye jina lake lifahamike kwa Watanzania, Bado Harmo Rapper anaendelea kutumia Kiki.

Juzi ameingia Mlango wa Kutokea baada ya Kupost Picha ya Muigizaji Malkia Nchini, Wema Sepetu na kudai kwamba ana hisia za Wazi za Kimapenzi kwa Wema na Yupo tayari kumuoa na kuishi naye kama Mume na mke kitu ambacho kimeonekana kumkera Wema Sepetu na Wema kuamua kumkata ngebe kupitia Instagram.

HUU HPA NI UJUMBE ALIOKUWA AMEUPOST HARMO RAPPER JUZI.

“Napenda kusema ukweli ulio jificha moyoni mwangu tangu siku nyingi kutokana na jinsi ninavyo sumbuliwa na hisia za kimapenzi kwa mrembo @WEMASEPETU,tangu naanza kumfaham wema sepetu na kumwona kweny tv akigombea umiss tz mwaka 2006 nilitokea kumpenda sana na kupata hisia za kumwoa endapo ntampata basi tu ndo vile nilikua sina uwezo wa kuonana nae wala kukutana nae kwa sababu ya position nilio kua nayo enzi hizo nauza pochi mwenge?nakumbuka kipind kile #WEMASEPETU wamemkata kweny uchaguz wa wabunge wa viti maalum niliumia sana,hadi skupatwa na usingiz nakumbuka niliamka saa 9 za usiku gheto na kuelekea mwenge kulangua mikoba kwa sababu ya kuiuza kipindi npo maeneo ya mwenge rafiki yangu alie kua na smart na alikua akifaham ni kiasigani namkubari #wemasepetunga alinipa taarifa kua #sepetunga anaingia dar kutokea dodoma baada ya jina lake kukatwa Ukwel nilisema lazima nikampokee na dhawadi nimpatie, bas nikaingia zangu kurangua mikoba nilibahatika kupata mkoba mmoja mzuri sana Akili ikanijia kua ule mkoba nmpe dhawad #kiumizaRohoYangu sikuuza nikauhifadh baadae nikafunga gori langu mapema nikaelekea kumpokea #kiumizaRohoYangu baada ya madam kufika niliangaika sana ili nimpatie ile dhawad ya mkoba bahati mbaya niligongwa na bodaboda kweny mguu wa kushoto na skufanyikiwa kumpa ila hadi leo ule mkoba nnao endapo siku nikipata fursa ya kukutana nae ntampatia huo mkoba.
Ila nachukizwa sana na vijana walio uchezea moyo wa #sepetunga wakina #Mrblue, #diamond,#idrisa na wengineo nawachukia sana kwa kuufanya moyo wa @WEMASEPETU kama danadana na kuwalaum juu.
Pia nawaonya wale wote mnao mlinganisha #Zarithebosslady na #WEMASEPETU mnakosea sana wema sepetu n mzuri mno kuliko #zarithebosslady sio kwamba #Mamatee n mbaya hapana mamatee ni mzuri ila hajamfikia #wemasepetu.
Yote ya yote naombeni mumfikishie Taarifa hizi #WEMASEPETU Mwambieni nampenda sana endapo nikampata hato chukua hata wiki kwangu ntamvisha pete na kufunga ndoa nae juu na kumtunza kwa hali yoyote ile.”

NA HIKI HAPA CHINI NDICHO ALICHOKIANDIKA WEMA SEPETU LEO

“Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae. Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao *DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO?* Usinidharaulishe…. Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but *AM NOT FOR U* and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako *LETS STOP THERE*”

Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae. Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao *DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO?* Usinidharaulishe…. Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but *AM NOT FOR U* and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako *LETS STOP THERE*

A post shared by Wema Sepetu (@wemasepetu) on

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu