Wizara ya Maliasili na Utalii ,imeomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 334.3 Kwa mwaka Wa fedha 2026/27 ili kutekeleza malengo ya vipaumbele mbalimbali vya sekta hiyo ambavyo vinavyolenga kuimalisha uhifadhi kukuza Utalii na kuongeza mchango Wa sekta kupitia uchumi Wa Taifa.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo ,Bungeni Jijini Dodoma na Waziri Wa Maliasili na Utalii DKT. ASHATU KIJAJI , ameliomba Bunge kuidhimisha kiasi Cha shilingi bilion 334.3 kwa matumizo ya fungu68 katika mwaka Wa fedha 2026/27.
DKT .KIJAJI,amesema kati ya fedha hizo shilingi 272,044,425,000 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida huku shilingi62,301,445,000.zikielekezwa kwenye utekelezaji Wa Miradi ya Maendeleo.
Pia ,amefafanua kuwà fedha ya matumizi ya kawaida zinajumuisha shilingi144,691,490,000 Kwa ajili ya mishahara ya watumishi pamoja na shilingi127,352,935,000 Kwa matumizi ya mengine ya Wizara na taaasisi zake.
Katika mwaka Wa fedha 2026/27 vipaumbele vingine ni kuimarisha
Utangazaji Wa Utalii wa ndani na nje ya Nchi Kwa kutumia mikakati mahususi ya masoko hususani katika masoko ya kimkakati na mapya ikiwemo mashariki ya mbali na mashariki ya kati.



