Rais wa zamani wa Marekani George H. Bush afariki dunia

In Kimataifa

Rais wa zamani wa Marekani George H. W. Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94. Mtoto wake wa kiume George W. Bush ambaye naye aliwahi kuwa rais kati ya mwaka 2001-2009, amethibitisha taarifa za kifo cha baba yake na kusema alikuwa mtu wa haiba ya hali ya juu. Kifo cha Bush kinafuatia kifo cha mke wake Barbara, aliyefariki dunia mwezi Aprili. Rais Donald Trump anayehudhuria mkutano wa viongozi wa G20 nchini Argentina, ametuma salamu za pole na kumsifu kuwa mtu aliyejitoa kwa familia yake na nchi. Salamu za pole pia zimetoka kwa rais wa zamani Barack Obama aliyesema Marekani imepoteza kiongozi mzalendo. George Herbert Walker Bush kutoka Republican, alikuwa rais wa 41 wa Marekani kati ya mwaka 1989-1993, wakati ambao aliiongoza nchi yake katikati mwa matukio muhimu ikiwemo kuanguka kwa ukuta wa Berlin na kuporomoka kwa Muungano wa kisovieti.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu