Rais wa Marekani Donald Trump katika hatua nyingine ya kigeugeu ametangaza kuwa mkutano wa kilele kati yake na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un utaendelea kama ulivyopangwa. Mkutano huo umepangiwa kufanyika tarehe 12 mwezi huu huko nchini Singapore dhamira kuu ikiwa ni kuifanya Korea Kaskazini iachane na mpango wake silaha za nyuklia.Siku nane tu baada Trump kuufutilia mbali mkutano huo kwa madai ya ujeuri wa wazi wa Korea Kaskazini rais huyo wa Marekani alimkaribisha mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la Korea Kaskazini Kim Jong Chol ofisini mwake katika ikulu ya White House. Rais Trump amesema ana imani kubwa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ana nia ya kweli ya kutaka kuziondoa silaha za nyuklia nchini mwake.



