Chama Kikubwa cha Wafanyakazi Afrika Kusini Chaunga mkono Rais Zuma Kujiuzulu

In Kimataifa

Chama kikubwa cha wafanyikazi nchini Afrika Kusini, Cosatu kimeunga mkono kauli ya wale wanaomtaka rais Jacob Zuma kujiuzulu.

Japo Cosatu kinajulikana kuunga mkono chama tawala ANC, kimemshutumu rais Zuma kwa kile wanachokitaja kuwa na uhusiano wa karibu mno na familia moja ya jamii ya Wahindi huko Afrika Kusini, waitwao Gupta, wanaodaiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika serikali ya Zuma.

Wiki iliyopita chama chengine mshirika wa ANC The South African communist party pia kilimtaka Bw. Zuma kung’atuka mamlakani kutokana na kashfa tele zinazozidi kumuandama, madai ya makosa ya ufisadi.

Sarafu ya Rand imekuwa ukiyumba yumba kutokana na malumbano hayo ya kisiasa nchini Afrika Kusini hasa tangu kufutwa kazi kwa aliyekuwa waziri wa fedha nchini humo Pravin Gordhan.

Wito wa Cosatu wa kumtaka kujiuzulu ni pigo kubwa kwa kiongozi huyo wa taifa.

Chama chicho cha wafanyikazi kimekuwa kikimuunga mkono dhidi ya wito wa kumtaka kung’atuka mamlakani.

Macho yote sasa yanaelekezwa katika kamati ya kazi ya chama cha ANC ambacho kinafanya mkutano.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu