Korea Kaskazini imefyatua Kombora Jingine na kulielekeza kwenda bahari ya Japani.
Kombora hilo lenye uzito wa kati limerushwa Katika Mji wa Pyongyang, upande wa mashariki mwa bandari ya Sinpo kuelekea bahari ya Japan.
Hata hivyo Waziri kiongozi wa nchi wa Japan, Yoshihide Suga ameongea na waandishi wa habari na kusema nchi yake haiwezi stahimili vitendo hivyo vya uchochezi ambavyo Korea kaskazini imevirudia kuvifanya.
Kombora hilo limerushwa siku chache kabla ya rais wa China, Xi Jinping kufanya ziara nchini Marekani kukutana na rais Trump ili kujadili namna ya kudhibiti mipango ya Nuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea kaskazini. .
