Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

In Kimataifa

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza, chombo cha habari chenye uhusiano na serikali kimeripoti Jumatano.

Mahakama imesema Ali Reza Akbari, ambaye alikuwa naibu waziri wa ulinzi hadi mwaka 2001, alikuwa “jasusi mkuu” wa idara ya ujasusi ya Uingereza, shirika la habari la Tasmin limeripoti.

Tasmin imeripoti pia kuwa alifanya ujasusi kwenye mazungumzo ya zamani ya nyuklia kati ya Iran na mataifa ya magharibi.

Akbari alihudumu kama naibu waziri wa ulinzi chini ya uongozi wa Rais Mohammad Khatami, mwanamageuzi ambaye alishinikiza kuboreshwa kwa uhusiano na nchi za magharibi.

Uingereza imeomba hukumu hiyo isitishwe na Akbari aachiliwe mara moja.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza James Cleverly amesema katika taarifa “ Hiki ni kitendo kilichochochewa kisiasa na utawala wa kikatili ambao unapuuza kabisa maisha ya binadamu.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya

Arsenal wana nia ya kumsajili nyota wa Barcelona Alejandro Balde huku beki huyo wa pembeni wa Hispania mwenye umri

Read More...

Somaliland yagundua Mafuta

Jamhuri iliyojitangaza ya Somaliland imetangaza kugunduliwa kwa kisima cha mafuta katika eneo la Salhayey eneo la Marodi-Jeh, wizara yake

Read More...

WAKAZI WA ARUSHA WAHIZWA KUTUNZA AMANI YA JIJI LA ARUSHA AMBALO NI KITOVU CHA UTALII NCHI

Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi Wananchi wa jiji la Arusha wamehimizwa kutunza amani na utilivu wa jiji hilo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu