Mwanamume mmoja kutoka Rongai anahuzunika baada ya
askofu wa kanisa lake kudaiwa kutoroka na mke wake katika
eneo lisilojulikana.
David Makori anadai kuwa Askofu Charles Maloba wa Kanisa
la Power Pentecost alimpkonya mkewe ambaye alikuwa ni
mwanakwaya wa kanisa hilo miezi mitatu iliyopita na sasa
wanaishi pamoja mahali pasipojulikana huko Kajiado.
Kulingana na Makori, juhudi zake za kurudiana na mke wake
ambaye wamezaa pamoja mtoto mmoja zimeambulia patupu.
Makori anasema kuwa mkewe alimwambia kwamba hawawezi
kuwa pamoja tena kwa sababu tayari amepata penzi kwa
Mtumishi wa Mungu ambaye pia ana mke wake.
Makori anadai kuwa huenda askofu huyo alitoroka na mke wake
ambaye wamekuwa pamoja kwenye ndoa kwa miaka 10,
kutokana na jinsi anavyoimba vyema katika kwaya ya kanisa.
Inaonekana askofu alipendezwa na uimbaji wake katika kwaya
na kuitumia kama njia ya kumsongeza karibu.



