Mbunge wa jimbo la Maswa magharibi Mhe Mashimba Ndaki,
ameitaka serikali kuja na mkakati wa kunusuru anguko la bei za
mazao ya wakulima Nchini kwa kuanzisha mfuko maalumu wa
ruzuku.
Mbunge Mashiba Ndaki ametoa ushauri huo leo juni 20 2023,
wakati akichangia mjadala wa bajeti kuu ya serikali kwa mwaka
wa fedha 2023/24 ambapo amesema kushuka kwa bei za mazao
kumekuwa kukiwakatisha tamaa wakulima/



