Benki ya biashara Afrika ( CBA) imezindua huduma mpya ya kibenki, inayomwezesha mteja kuhudumiwa
kibinafsi popote pale alipo, kwa kupewa vipaumbele tofauti badala ya kufuata huduma hiyo benki.
Aidha huduma hiyo ambayo ni tofauti inamsaidia mteja kupata huduma zote za kibenki kibinafsi, na kuondoa changamoto kubwa iliyokuwepo ya wateja kutoka mbali na kufuata huduma hiyo.
Akizungumza wakati wa kuzindua huduma hiyo jijini Arusha, Mkurugenzi wa benki hiyo nchini Tanzania, Gift Shoko amesema kuwa, huduma hiyo itakuwa inafanya kazi katika mikoa ya Arusha, Dar es salaam, na Mwanza.
Shoko amesema kuwa, lengo la kuanzisha huduma hiyo, ni baada ya kugundua watu wengi wanakosa nafasi kutokana na majukum, kwa maendeleo ya nchi na kuwafanya kukosa muda wa kufika benki , hivyo wameona umuhimu wa kuwafikia pale walipo, katika kupata huduma mbalimbali muhimu.
Mwenyekiti wa benki hiyo Ndewirwa Kitomari , amesema kuwa, CBA ndio benki ya kwanza kutoa mikopo ya nyumba, ambapo wamejiwekea mikakati ya kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wajasiriamali huku wakijikita zaidi katika kukuza uchumi wa viwanda.
benki ya CBA ambayo ilianzishwa mwaka 1962 ina jumla ya matawi 11 nchini, ambapo ipo pia katika nchi za Afrika mashariki ambazo ni Kenya, Uganda na Rwanda
