Bundesliga kuanza tena wikendi hii.

In Kimataifa, Michezo

Ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, inarejea tena mwishoni mwa juma baada kusitishwa kwa karibu miezi miwili kutokana na janga la virusi vya corona.

Kuanza tena kwa ligi hiyo kunaangaliwa kama jaribio juu ya iwapo kandanda na mashindano mengine ya michezo duniani yanaweza kuanza tena chini ya kiwingu cha janga la COVID-19.

Miongoni mwa michezo ya kufungua dimba itayofanyika kesho ni pamoja na mpambano wa kukata na shoka kati ya mahasimu wa jadi Borussia Dortmund na Shalke 04 mjini Dortmund.

Hata hivyo mechi tisa za duru ya 26 ya Bundesliga zitachezwa bila kuwepo mashabiki uwanjani.

Ligi nyingine barani Ulaya ikiwemo ile ya Uingereza, Italia na Uhispania zinatarajiwa kuanza tena baadae mwezi Juni.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza,

Read More...

Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuuJackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wawashirika wawili ambao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu