Bunge kupiga kura tena 29 mwezi januari.

In Kimataifa

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ataitisha kura nyingine Januari 29 kuhusu makubaliano ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya, kufuatia kushindwa vibaya katika kura ya kwanza mapema wiki hii. Kiongozi wa chama cha Conservative katika baraza la wawakilishi Andrea Leadsom, amesema kura hiyo itafuatia mjadala kuhusu hatua zijazo za serikali kuhusu makubaliano ya Brexit. Leadsom ameliambia bunge kuwa tamko na muswada kuhusu hatua zinazofuata za serikali vitawasilishwa siku ya Jumatatu, na kuongeza kuwa mjadala wa siku nzima kuhusu muswada huo utafuatia Januari 29. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas hata hivyo amewataka wenye dhamana ya kisiasa nchini Uingereza kuacha maneno na kuwajibika:May alipoteza kura siku ya Jumanne kuhusu makubaliano yake ya Brexit kwa rekodi ya kura 230, baada ya wabunge wa chama chake cha Conservative wanaounga mkono kubakia katika Umoja wa Ulaya na wanaotaka kujiondoa kuungana na wabunge wa vyama vya upinzani kupiga kura dhidi ya mpango huo. Ameahidi kutafuta muafaka bungeni kwa kufanya mikutano na wabunge wa chama chake pamoja na wa upinzani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu