DR. MOLLEL ATOA PONGEZI KWA WAUGUZI WALIOJITOA KATIKA AJALI YA NDEGE

In Kitaifa

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewashukuru Watumishi wa afya wote walijitokeza kuhudumia majeruhi katika ajali ya ndege iliyotokea katika Mkoa wa Kagera iliyotokea Novemba 6, 2022.

Dkt. Mollel ametoa pongezi hizo leo Novemba 8, 2022 alipowatembelea majeruhi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ambapo kwa jitihada za Watumishi wa afya mpaka kufikia leo alibaki majeruhi mmoja tu.

Aidha, Dkt. Mollel amesisitiza Serikali itaendelea kugharamia majeruhi wote waliotokea katika ajali hiyo ya ndege mpaka watakapokuwa sawa kiafya.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali afya za Watanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu kama majengo ya dharura na kuwapa mafunzo Wataalamu ambao kwa kiasi kikubwa wamesaidia katika kuokoa hali ya majeruhi waliokuwa katika ajali ya ndege.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu