ECOWAS kukutana Abuja kujadili mapinduzi nchini Niger.

In Kimataifa

Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa jumuia ya uchumi ya mataifa ya Afrika magharibi (ECOWAS) wanakutana katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kuanzia leo Jumatano hadi Ijumaa kujadili mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, jumuiya hiyo imesema.

Siku ya Jumapili, ECOWAS iliiwekea vikwazo Niger na kuonya kuwa inaweza kutumia nguvu huku ikiupa utawala wa kijeshi muda wa wiki moja kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum.

Afisa wa ECOWAS pia aliiambia AFP jana Jumanne kwamba ujumbe wa jumuiya hiyo unaoongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Abdulsalami Abubakar utafanya ziara Niger leo Jumatano.

Mapinduzi hayo yamezitia wasiwasi nchi za magharibi zinazojitahidi kudhibiti uasi wa wanamgambo wa kiislamu uliozuka kaskazini mwa Mali mwaka 2012, na kuingia Niger na Burkina Faso miaka mitatu baadaye na sasa unatishia mataifa dhaifu katika Ghuba ya Guinea.

Raia kadhaa, wanajeshi na polisi wameuawa katika eneo hilo lote, wengi katika mauaji ya kikatili, huku watu milioni 2.2 nchini Burkina Faso pekee wakiwa wamehama makazi yao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

DC Magoti apiga Marufuku pikipiki kubeba mkaa.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ndugu PetroMagoti,amepiga marufuku piki piki kubeba mkaa katika Wilayahiyo kuanzia leo July

Read More...

Hali ilivyo Kenya sasa baada ya maandamano

Baada ya maandamano yaliyofanyika nchini Kenya juu ya Muswa wa sheria ya Fedha,leo tumezungumza na ndugu Daniel Orogo mchambuzi

Read More...

Rais wa Msumbiji kufungua maonesho ya sabasaba

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji ambaye anatarajiwa kuwasili nchini kesho kuanza ziara ya kikazi, anatarajiwa kufungua rasmi Maonesho ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu