Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa Tume ya Ushindani ( FCC) Khadija Ngosongwa, amesema kuwà katika robo ya kwanza na ya pili malalamiko 63 yameshughulikiwa kati ya 45 yalipatiwa ufumbuzi na malamiko kumi na Tisa yalibaki yapo katika hata mbalimbali za utatuzi.
Ngosongwa,amesema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na wahandishi Wa habari kuhusu Utekelezaji Wa Miradi ya maendeleo na frusa za Vijana kwa mwaka 2025/2026 Kwa tume hiyo Kwa serikali ya awamu ya sita.
Pia ,amesema taasisi za kifedha hasa sekta ya Mikopo ya kifedha ambazo zinaruhusiwa kuongeza riba au kufanya mabadiliko katika programu yao bila kupitia Tume ya Ushindani Kwa mujibu Wa taratibu zilizowekwa.
Amesena, Tume ya hiyo imekuwa ikifanya ushirikiano mkubwa na Benk kuu ya Tanzania Kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali na kujadili namna ya kuwalinda walaji hasa katika sekta za kifedha ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi.
Kwa upande mwingine ,amesema katika kipindi cha mwaka 2025/26, Tume ya Ushindani iliridhia ununuzi wa makampuni mawili katika sekta ya kilimo yenye thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 20.4. Uamuzi huo ulilenga kuyawezesha makampuni hayo kupanua wigo wao sokoni, kuongeza mitaji, na kuepusha hatari ya kuondoka sokoni.
Ameongeza kusema , moja ya makampuni hayo ni Africado Limited, linalojishughulisha na uzalishaji na usafirishaji wa maparachichi katika masoko ya kimataifa, ambalo lilinunuliwa na AgDevCo Limited kwa ushirikiano na Garth John Weston.
Tume ya Ushindani FCC ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa Kwa mujibu Wa kifungu Cha 62(1) Cha Sheria ya Ushindani (Na 8 ya mwaka 2003 kama yalivyorekebishwa Sheria ya ushinda I) Kwa madhumuni ya kukuza na kulinda Ushindani katika biashara na kulinda mlaji dhidi ya mienendo hadaifu na kandamizi katika uchumi Wa soko



