FIRM BEGINNINGS FOUNDATION KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI

In Kitaifa

Vijana 100 kutoka shule za sekondary jijini Arusha , wamekutanishwa na Taasisi Vijana ya inayojihusisha na kutoa ujuzi maarifa, pamoja na kushirikishana uzoefu ijulikanayo kama FIRM BEGINNINGS FOUNDATION iliyopo Jijini Arusha 
Akizungumza na Waandishi wa  Habari wakati wa mafunzo hayo ambayo yamewashirikisha vijana wa kidato cha Sita kutoka shule 3 za sekondary jijini Arusha Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Joycelyne Umbulla alisema kuwa lengo la kuwakutanisha ni ili kuwajengea uwezo wa kijitambua ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo mbalimbali kutoka kwa wadau wa maswala ya maendeleo ili waweze kuhamasika kufanya uchaguzi sahihi wa kazi wanapoingia vyuo 
Umbulla alisema kuwa taasisi hiyo anawasaidia vijana ambao wako Mashuleni na wale ambao hawapo mashuleni ambapo ambao wako mashuleni ni wa kidato cha nne kuingia cha Sita, ambao wanatarajia kuingia elimu ya juu, pamoja na vijna ambao waliacha masomo kwa sababu mbalimbali 


Alisema kuwa, warsha hiyo Ilianza na vijana 100 ili waweze kufahamiana, kubadilishana, mawazo na pia Aliwaalika wataalamu kutoka taaluma ya Sheria, fedha, Afya , na Biashara ili vijana waweze kupata majibu sahihi ya wataalamu hao ili waweze kupata mawazo chanya katika kujifunza mambo wanayoyahitaji katika maisha yao.
Kwa upande wao wataalamu walioshiriki kuwaelimisha wanafunzi hao akiwemo Mtafiti  wa maswala ya kinga ya mwili katika Taasisi ya Afya ya Ifakara Dr. Anneth Tumbo, Wakili Elibariki Maenda, na Mr. Zablon Mgonja walisema   warsha hiyo ni nzuri sana na itawasaidia vijana hao kuweka kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao na kuwa na utambuzi wa kubadilisha maisha yao, familia yao, lakini pia kwa nchi yao.


Walisema kuwa taasisi kama hizo zinapaswa kupewa ushirikiano kutoka Serikalini kwani Zainaisaidia serikali hasa katika kutoa michango mbalimbali ya mawazo yao na vitendeakazi pale wanapohitaji
Nae Mgeni Rasmi katika Warsha hiyo ambaye ni Youth Development Regional, Admisrtation, and Local Government Mr. Japhet Kurwa aliipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri ya kuwajengea uwezo vijana hao kwani serikali ya Jamuhuri ya Anuu gani wa Tanzania inatambua mchango mkubwa wa vijana na kuahidi kuungana nao katika kuhakikisha wanatimiza Malengo yao. 
Kwa Upande wao vijana waliobahatika kushiriki warsha hiyo Akiwemo Kefrick Shimwela,Frank Masanja,Caroline Bethuel, na John Richard walisema kuwa Semina hiyo imewabadilisha na wamejifunza mambo mengi hivyo wameahidi kusambaza elimu waliyoipata kwenda kuwafundisha wenzao ambao hawakuhudhuria 


Hata hivyo Warsha hiyo imezijumuisha Shule za Ilboru, Arusha Sekondary, na Arusha Girls

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu