Bondia maarufu Floyd Mayweather alitangaza moja ya mali zake za gharama na kutaja bei ambayo kama mtu yeyote angekuwa na uwezo angemuuzia.
Kupitia mtandao wa wa biashara za online eBay tarehe 31 ya mwezi uliopita akaunti rasmi ya Mayweather ilipandisha picha ya gari lake la gharama aina ya “Bugatti Grand Sport Vitesse ya mwaka 2015′ iliyotangazwa kuuzwa dola millioni za kimarekani 3.95 ambayo ni sawa na Tsh bilioni 8.8.

Muonekano wa gari hilo nje na ndani
Floyd amekuwa ni mtu wakumiliki vitu vya gharama na inawezekana kabisa aliweka gari hilo mtandaoni kujiingizia pesa kupitia umaarufu kwa kuwa wengi wangetamani kumiliki gari hilo ambalo ameshalitumia.
Hata hivyo gari hilo mwisho wa biashara hiyo ilikuwa ni tarahe 5 ambapo hakuna mtu aliyeweza kufikia dau hilo.
