Halmashauri ya jiji la Mbeya ipo katika mikakati ya ujenzi wa kituo cha
mabasi cha kisasa katika eneo la uwanja wa ndege wa zamani.
hayo yamesemwa na mstahiki meya wa jiji la mbeya DourMohamed Issa
ambapo amesema tayari wamekamilisha mchakato wa kupata fedha za mkopo
kutoka benki ya dunia.
Aidha ameongeza kuwa tayari wamempata mkandarasi ambae atashughulika
na ujenzi huo.
Pamoja na hayo amesema wataboresha miundo mbinu ya barabara ndani ya jiji
la mbeya.


