MWENGE wa uhuru umezindua mradi

In Kitaifa

MWENGE wa uhuru umezindua mradi wa kuhifadhi mazingira wa shule
ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara wa wenye thamani ya shilingi 18,210,000.


Mkuu wa shule ya sekondari Mgutwa Donald Lema akisoma taarifa ya
mradi huo kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu
Sahili Nyanzabara Geraruma, amesema mradi huo una miti 2,150
iliyopandwa.


Mwalimu Lema amesema matarajio yao kwa mwaka huu ni kupanda
miti ya matunda 350.
Amesema wanaamini mradi huo unachangia katika kupunguza kiasi cha
hewa ya ukaa kilichopo angani na kufanya eneo hilo kuwa mahalo
pazuri zaidi kwa maisha ya binadamu na viumbe wengine hai.


Amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 131ikiwa idadi ya
wasichana ni 63 , wavulana 68 na walimu saba.


Amesema shule hiyo ilitembelewa na mwenge wa uhuru mwaka jana na
kuona mradi huo upandaji miti na utunzaji mazingira.


Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu, Sahili Nyanzabara
Geraruma ameipongeza shule ya sekondari Mgutwa kwa kufanikisha
mradi huo wa kuhifadhi mazingira.


Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera amesema mwenge
ukiwa wilayani humo  utatembelea miradi sita ya thamani ya shilingi
bilioni 1.3.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu