Mwanaume mmoja mwenye miaka 25 anapatiwa matibabu
katika Hospitali ya Kyuso Level 4 kaunti Ndogo ya Mwingi
nchini Kenya kwa kula sumu, baada ya kumuua mama yake
mzazi mwenye miaka 58.
Kimanzi Muthui anaripotiwa kumchanachana Agnes Kisyinoi na
panga baada ya kukataa kumpa chakula cha jioni usiku wa
Jumatatu Mei 26 mwezi uliopita hapo.
Kulingana na polisi nchini humo mshukiwa aliwasali nyumbani
na kumuamuru mama yake ampakulie chakula lakini marehemu
alikataa na wakaanza kugombana.
Mshukiwa anasemekana alichukua panga na kumkata kata
mama yake mara kadhaa katika sehemu tofauti za mwili na
kusababisha kifo chake papo hapo.
Baada ya kufanya tukio hilo kijana huyo alikunywa sumu
akijaribu kijiua,lakini aliokolewa na majirani ambao
walimpeleka Hospitali.
Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka mawili kwanza la mauaji ya
mama yake na la pili kutaka kujiuwa.
