Kulia ni jambo la kawaida katika binadamu na kulia huko
kunaweza kuchangiwa na hali tofauti.
Watafiti wengi wamegundua kuwa kulia kunaweza kuleta
manufaa makubwa zaidi katika mwili wako na akili zako, na
manufaa haya huanzia wakati wa kuzaliwa anapolia mtoto.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Wataalamu wa Jicho ya Florida na
Watoto-Macho, kuna nyakati mbalimbali ambako hisia
huonyeshwa kupita machozi.
Kwa mujibu wa jarida la Medical News Today, wanawake hulia
mara nyingi zaidi kuliko wanaume, kwa wastani wa mara 3.5
kwa mwezi na wanaume mara 1.9 kwa mwezi.
Kuna aina tatu za machozi:
Machozi haya husababishwa na hali tofauti na kila chozi lina
mchanganyiko wake.
Machozi ya Msingi-Machozi haya kwa lugha ya kiingereza ni
Basal na hutolewa na vifereji vya machozi na huwa na madini
mengi ya protini.
Pia yanauwezo na nguvu za kupambana na bacteria na kila mara
unapopepesa macho, aina hii ya machozi husaidia jicho kuwa
majimaji.
Machozi ya Hisia-Aina hii ya machozi hutokea kutokana na
hali mbalimali za hisia na mchanganyiko wake huwa na homoni
nyingi za mfadhaiko kuliko machozi mengine.
Husaidia sana katika kutuliza uchungu au maumivu,yanaweza
kuwa na protini na homini ambazo hazipatikani katika machozi
ya msingi ama yale ya mwitikio wa ghafla.
Machozi ya Mwitikio wa ghafla-Aina hii ya machozi
husababishwa na mwasho, mfano wa vitunguu, moshi ama
upepo.
Kazi ya machozi hayo ni kuondoa mwasho huo ili kulilinda
jicho na hutoka mengi kuliko machozi ya msingi, na huenda
yakawa na kinga mwili ambazo husaidia kupambana na
bakteria.
