Viongozi wa kijeshi wa Sudan wametangaza makubaliani na muungano wa upinzani juu ya kipindi cha mpito cha miaka mitatu kwa ajili ya kuukabidhi utawala wa kiraia.
baraza la kijeshi la mpito (TMC) limesema kuwa muungano utakuwa na theruthi mbili ya viti katika baraza la bunge.
Sudanimekuwa ikitawaliwa na baraza la jeshi ltangu mwezi uliopita baada ya mapinduzi ya rais Omar al-Bashir.
Maandamano yaliyosababisha kuanguka kwa utawala wake yamekuwa yakiendelea huku waandamanaji wakidai kuwekwa kwa serikali kamili ya kiraia.
Saa kadhaa kabla ya mkataba wa sasa kutangazwa, takriban waandamamnaji watano na afisa mmoja wa usalama walikufa katika makabilianokatika mji mkuu Khartoum.
Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Luteni Jenerali Yasser al-Atta alisema kuwa makubaliano ya mwisho juu ya mgawanyo wa madaraka yatasainiwa pamoja na upinzani – Azimio la the Declaration of Freedom na Change Forces (DFCF) – katika kipindi cha saa 24. makubaliano hayo yatajumuisha kubuniwa kwa baraza la kujitawala ambalo litaongoza taifa mpaka uchaguzi utakapofanyika.
“Tunaapa kwa watu wetu kwamba makubaliano yatakuwa yamekamilika katika kipindi cha saa 24 kwa njia inayotarajiwa na watu,” alisema.



