Kamera ya kupiga picha ndani ya mwili wa binadamu yagunduliwa.

In Kimataifa, Tekinolojia

 

Wanasayansi wamebuni kamera yenye uwezo ya kupiga picha viungo vya ndani ya mwili wa binadamu.

Kifaa hicho kimeundwa kuwasaidia madaktari kusaka vifaa vya madaktari, vinavyofahamika kama endoscopes, amvayo huenda vinaweza kusalia ndani ya viungo vya binadamu wakati wa upasuaji.

Hadi sasa, matabibu wamekuwa wakitegemea uchunguzi unaogharibu fedha nyingi,kama vile picha za X-ray, ili kufuatilia mafanikio yao.

Kamera hiyo mpya, itafanya kazi ya kubaini mwanzo wa mwangaza ndani ya mwili wa binadamu, kama vile sehemu ya ncha ya mwisho ya kifaa cha upasuaji cha tube ya endoscope.

Profesa Kev Dhaliwal, wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, anasema: “Ina uwezo mkubwa wa kutumika katika hali tofauti tofauti, kama vile inavyoelezwa ikiwa kazini. “Uwezo wa kuona iliko kifaa kilichosahaulika ndani ya mwili wa binadamu hasa katika sekta mbalimbali ya kitengo cha kiafya, huku tukisonga mbele kupunguza hali na mbinu ya kila aina ya kutibu maradhi mbalimbali.”

’tishu na viungo’

Majaribio ya awali, inaonyesha kifaa cha prototype, kinaweza kubaini na kufuatilia mwangaza kupitia eneo la mshipa wa sentimita 20, katika hali tu ya kawaida.

Miali ya mwangaza kutoka kwa endoscope, inaweza kupenyeza ndani ya mwili, lakini mara nyingi hutawanyika au kuangazia nje ya mshipa na viungo, badala ya kupernyesa moja kwa moja mwilini.

Hali hii inatatiza hali ya kupata picha halisi ya iliko kifaa kilichoachwa mwilini.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu