Njiwa aliyetumiwa kusafirisha mihadarati apigwa risasi.

In Kimataifa

Polisi nchini Argentina wamempiga risasi njiwa ambaye alitumiwa kusafirisha mihadarati kwenda gereza moja nchini humo, kwa mujibu wa mamlaka za gereza hilo.

Njiwa huyo alionekana akiruka hadi kwenye uwanja wa gereza hilo, lililo katika mji wa Santa Rosa.

Maafisa waligundua kuwa ndege huyo alikuwa amefungiwa mfuko mdogo kwenye mgongo wake, uliokuwa na vidonge vya madawa ya kulevya.

Njia hiyo ya kusafirisha madawa ilikuwa imegunduliwa, na ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi.

Gazeti la Clarin lilichapisha picha ya njiwa huyo akiwa na mfuko mweupe, uliokuwa na tembe 44 za madawa ya kulevya.

Magereza nchini Argentina yalionya mwaka 2013 kuwa, walanguzi wa madawa ya kulevya walikuwa wakitumia njiwa waliokuwa wakifanya safari mara 10 hadi 15 kwa siku.

Watu watatu walikamatwa na njiwa 15 kupatikana, baada ya uchunguzi wa mwaka 2013.

Mapema mwaka huu njiwa ambaye alikuwa na mfuko uliokuwa na tembe 178 za dawa ya kulevya, alishikwa nchini Kuwait karibu na mpaka na Iraq.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu