Wakati imetoka Album ya Kanye West The Life of Pablo Watu wengi waliichukulia poa kwasababu ya kuchoka kuisubiri ambapo Kanye West aliahirisha mara kibao kuitoa huku akibadili jina zaidi ya mara 3 mwishowe akitoa kwa jina hilo.
Alichokifanya cha tofauti ni kwamba Album hiyo aliiachia Mtandaoni Pekeee watu wakasema atafell zaidi ila imekuwa Tofauti kwani Album hiyo imeweka Record Kubwa Duniani.
Recording Industry Association of America, RIAA. Imeiitangaza Album ya The Life of Pablo kuwa album ya kwanza iliyotoka mtandaoni pekee kwenda platinum.
Kwa mujibu wa label yake, Def Jam, Kanye amepata cheti cha platinum baada ya album hiyo kusikilizwa mtandaoni mara bilioni 3, kutosha kuifanya ifikie sawa na units milioni moja za mauzo ya kawaida.
HII HAPA CHINI NDIYO POST YA DEF JAM RECORDINGS Waliyopost kwenye Mtandao wa Twitter:-
