KATIBA YA CCM YAFANYIWA MABADILIKO 

In Kitaifa, Siasa

Kwa mujibu wa taarifa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na kufanya mabadiliko madogo katika Katiba ya CCM ambapo sasa Katiba hiyo inatambua ufanywaji wa mikutano ya ngazi mbalimbali kwa njia ya mtandao maarufu kama E- Meeting.

Dkt. Samia wakati akitangaza mapendekezo hayo kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Mabadiliko hayo ni katika kuhakikisha kuwa Chama hicho kinaenda sawa na mabadiliko mbalimbali ya teknolojia yanayotokea duniani,suala ambalo limewezesha CCM pia kufunga Mitambo ya teknolojia yenye kuwezesha Ngazi za CCM wilaya na Mikoa kuweza kuunganishwa pamoja na Makao Makuu kwa njia ya mtandao.

Amebainisha kuwa Idara ya Oganaizesheni ilipendekeza vikao vitakavyoweza kufanyika kimtandao ni Vikao vya Sekretarieti ya Wilaya, Kamati za siasa za wilaya, Sekretarieti za Mikoa, Kamati za siasa za Mikoa, sekretarieti ya Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kamati Maalum ya halmashauri kuu ya CCM Taifa,Halmashauri kuu ya CCM Taifa pamoja na Mkutano Mkuu wa Taifa.

“Vikao husika vitafanyika kwa njia ya mtandao endapo tu kuna ulazima, vikao husika kwa ngazi ya Mkoa vitafanyika kwa idhini ya Katibu Mkuu. Watamjulisha Katibu Mkuu kwanini wafanye kikao kwa mtandao na hii ni kuepusha kutumika vibaya kwa mitandao hii.” Ameongeza Dkt. Samia.

Mabadiliko mengine ya Katiba yaliyofanywa na Mkutano Mkuu wa CCM Leo Alhamisi ni pamoja na Kuongeza idadi ya mabaraza ya wadhamini kutoka nane hadi tisa pamoja na mabadiliko madogo ya kutaka miradi ya maendeleo inayotekelezwa ngazi ya Mikoa kukasimiwa kwa maandishi kwenye ngazi hizo.

ReplyForwardAdd reaction

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

NIFFER NA CHAVALA WAACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewaachia huru leo mchana vijana Jennifer Jovin (26), maarufu kama

Read More...

Trump kukutana na viongozi wa Rwanda na DR Kongo Alhamisi

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Alhamisi

Read More...

SERIKALI YAAGIZWA KUFUTWA KWA LESENI 73.

Serikali kupitia Wizara ya Madini imeielekeza Tume ya Madini kufuta jumla ya leseni 73ambazo maeneo yake hayajaendelezwa. Hayo yameelezwa leo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu