
Mwanamitindo Maarufu Duniani na Mama wa Watoto Wawili, Kim Kardashian ambaye ni mke halali wa Rapper wa Marekani, Kanye West, Amefunguka Mapya yanayomfanya aendelee kuwa Bora kila wakati kwenye Suala Zima la Mitindo.
Mwanamitindo huyo amesema Siri kubwa aliyoihifadhi moyoni mwake inayomfanya aendelee kuwepo on Top kwa Wanamitindo, ni Kukubali kuyapokea yote mabaya na Mazuri anayotupiwa huku yeye akiyatumia kama Mafunzo kwake.
Kim amesema kuna wakati watu wanamtukana kiasi ambacho angekuwa na Moyo Dhaifu angeshakata tamaa lakini kutokana na Kujiamini kwake na kile anachokifanya yeye anachukulia kama Shule.
Kim Kardashian anaendelea kuweka tishio kwenye Tasnia ya Mitindo kwa kuingiza Sokoni Beauty line yake mpya aliyoipa jina la KKW
KAMA WEWE NI MWANAMITINDO BILA SHAKA UTAKUWA UMECHUKUA KITU HATA KIMOJA
