Mabilioni ya Escrow yaliyotoroshwa sasa kurejeshwa nchini.

In Kitaifa

Timu kabambe ya uchunguzi ikiongozwa na wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa itahakikisha kila senti iliyofichwa nje ya nchi inarejeshwa ili haki iweze kutendeka kwa wahusika.

Msako huo wa nchi za nje unatokana na kuwepo kwa taarifa za baadhi ya wanufaika wa mgawo wa mabilioni hayo kuwa walitoroshea fedha hizo barani ulaya na maeneo mengine mbalimbali duniani.

Aidha, harakati hizo za uchunguzi zinalengo moja tu kwamba hakuna fedha inayohusishwa na tuhuma hiyo ambayo haitafikiwa ikiwa ni pamoja na zile zilizokuwa zikizungumziwa bungeni zilizochotwa kwenye benki kwa mifuko ya sandarusi na ile ya rambo.

Imeelezwa kuwa eneo kubwa ambalo limelengwa na uchunguzi huo ni bara la Ulaya ambako inasemekana ndio kuna kiasi kikubwa cha fedha kimehifadhiwa na wanufaika wa mgawo huo.

Mussa Misalaba Ofisa Mahusiano wa Takukuru amesema kuwa ni kweli tuna maofisa wetu wa takukuru wamekwenda nje ya nchi kufuatilia fedha za Escrow, kwa sasa siwezi kutaja kuwa ni nchi gani hasa tunazozifuatilia maana huu ni uchunguzi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa taasisi hiyo ya Takukuru imeamua kushirikisha taasisi zingine za Kimataifa katika kuwachunguza zaidi baadhi ya watuhumiwa wa Escrow kama wamehifadhi fedha hizo nje ya nchi.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu