KIVUMBI UCHAGUZI ANGOLA

In Kimataifa, Siasa

Tume ya uchaguzi ya Angola imesema asilimia 86 ya kura zote tayari zimehesabiwa, ambapo zinaonyesha kuwa Chama tawala cha Kikomunisti cha zamani Angola, MPLA kina uwezekano wa kuendeleza utawala wake kwa muongo wa tano – ikimpa Rais Joao Lourenco kipindi kingine cha miaka mitano.

MPLA imetawala Angola kwa takriban miaka 50 baada ya nchi hiyo kupata uhuru kutoka utawala wa Ureno. MPLA ina utamaduni wa kudhibiti mchakato wa uchaguzi, na vyombo vya habari vya serikali na upinzani na makundi ya kiraia vimeeleza wasiwasi wa upigaji kura kuchakachuliwa.

Wakazi wa Luanda wameonyesha hisia mseto za hesabu ya kura ya awali ambayo iliripotiwa kwa upana zaidi na vyombo vya habari vya ndani ya nchi, huku ukurasa wa mbele wa gazeti la serikali Jornal de Angola la Alhamisi likisema: “MPLA inaongoza katika hesabu ya kura.”

Kiongozi wa chama cha upinzani UNITA Angola Adalberto Costa Junior.
Kiongozi wa chama cha upinzani UNITA Angola Adalberto Costa Junior.

Chama cha Upinzani cha UNITA, kinachoongozwa na Adalberto Costa Junior, hakikujibu mara moja ripoti hiyo. UNITA imepuuza matokeo ya awali yaliyotangazwa mapema na tume siku ya Alhamisi yakisema siyo ya kuaminika.

Mgombea nafasi ya makamu wa rais kwa tiketi ya UNITA Abel Chivukuvuku amekiambia kituo cha radio cha TSF kuwa chama hicho kinafikiria kupinga matokeo ya uchaguzi kwa sababu “hayalingani na ukweli ulivyo,”

“Nimekipigia kura chama cha UNITA, na siamini matokeo haya,” alisema Jorge, 40, fundi magari ambaye hakutoa jina lake la pili, akiishutumu tume ya uchaguzi kwa kula njama na chama tawala.

“Nahisi vibaya sana. Nchi haiwezi kupata mabadiliko, ni hadithi ile ile kila siku.”

Raia mwingine wa Angola, mhandisi Jose Viera Manuel, pia ana mashaka kama kura italeta mabadiliko.

“Kwa kweli mwisho wa siku sisi tumesikitishwa kwa sababu iwapo hali hii itabakia ilivyo, idadi yote itaongezeka zaidi kwa vile walivyo hivi sasa, kwa sababu wao wako madarakani, wana zana za kuchakachua uchaguzi na sisi sote tunajua watakuja kufanya hili mwisho wa siku,” Manuel alisema. “Kuna uwezekano wakachakachua, unajua hilo.”

Wachambuzi wa kisiasa wameona uchaguzi wa Jumatano kama ni fursa bora kabisa ya kipekee kwa ushindi wa UNITA wakati kukiwa na ongezeko la hasira za vijana wa Angola kuwa wametengwa katika kunufaika na utajiri wa mafuta wa nchi yao. MPLA imekuwa ikitawala tangu Angola ilipopata uhuru kutoka Ubelgiji mwaka 1975.

Tangazo la matokeo ya awali lililofanywa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (CNE) ilishangaza uharaka wake baada ya upigaji kura kukamilika – matokeo huko nyuma yalikuwa yanachukuwa siku kadhaa. Mwaka 2017, matokeo ya mwisho ya uchaguzi yalitangazwa wiki mbili baada ya upigaji kura kukamilika.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu