Kocha wa Hard Rock ataja sababu za kubamizwa na Simba.

In Kitaifa, Michezo

 

Baada ya kushuhudia timu yake ikiambulia kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba, Kocha wa timu ya Hard Rock, Muhibu Kanu amesema wachezaji wake walikuwa na hofu.

 

Kanu amesema mchezo huo umemsaidia kuona wapi ambapo kuna mapungufu katika kikosi chake, ambapo atayafanyia kazi lakini akadai kuwa wachezaji wake walikuwa na hofu kwa kuwa waliona wanacheza na timu kubwa.

 

Alidai kuwa ameona mapungufu na kwa kuwa ligi ya Zanzibar inatarajiwa kuanza hivi karibuni, anaamini Simba ilikuwa ni kipimo kizuri kwa wachezaji wake na benchi lao la ufundi limeshaona upungufu ulipo.

 

“Sijalia kufungwa kaisi kikubwa cha mabao, lakini naamini wachezaji wangu watakua wamejifunza kitu,na kwa upande wangu nimeona mapungufu yapo wapi, na ninaahidi nitayafanyia kazi ili kufanya maboresho.

 

“Wachezaji wangu walionyesha uoga dhidi ya wapinzani wao, na hii walijitengenezea mazingira ya kuogopa tangu mwanzo, kwa sababu ya jina la timu pinzani ya Simba, lakini bado hilo ni tatizo ambalo nimelibaini, nitalifanyia kazi ili kuwarejesha wachezaji katika saikolojia ya kupambana, na sio kuogopa jina”. Amesema Kanu

 

Mchezo wa jana ulikua wa kwanza kwa kocha Muhibu Kanu tangu alipomaliza masomo ya ukocha mkoani Morogoro, na anatarajia kukiongoza kikosi chake cha Hard Rock kwenye mshike mshike wa ligi ya Zanzibar ambao umepangwa kuanza Oktoba Mosi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu