Tambwe, Chirwa wawatuliza yanga Jumamosi hii Njombe.

In Kitaifa, Michezo

Washambuliaji wa kutumainiwa wa Yanga, Obery Chirwa pamoja na Amissi Tambwe leo hii wataungana na kikosi hicho katika mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga na Njombe Mji zitapambana Jumamosi hii katika Uwanja wa Sabasaba mijini Njombe baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kuifanyia mabadiliko ratiba ya ligi kuu ambapo awali ilikuwa zipambane Jumatano hii. Kitendo hicho cha nyota hao kujiunga na kikosi hicho kimepokelewa kwa mikono miwili na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo baada ya kuwakosa kwa kipindi kirefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti.

Majeraha hayo yaliwafanya wawe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu huku wakishindwa kuitumikia timu yao hiyo katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba lakini pia ule wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC.

Mechi zote hizo Yanga haikufanya vizuri.Akizungumza na Championi Jumatatu, Daktari wa Yanga, Edward Bavu, alisema kuwa wachezaji hao kwa pamoja leo hii wataanza mazoezi baada ya kupona majeraha yao.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu