Kumhamishia Mtoto Kwenye Chumba Chake

In Mahusiano

Wazazi wengi wamezoea kulala chumba kimoja na mtoto wao pale ambapo amezaliwa hadi kufikia umri fulani. Wengine huwa wanalala nao kitanda kimoja na wengine wanakuwa na kitanda cha mtoto pembeni ya kitanda chao. Kila mzazi anawakati wake ambao anaona ni vyema kumhamisha mtoto kwenda kwenye chumba na kitanda chake. Zoezi hili mara nyingi huwa ni gumu maana mtoto alizoea kulala na watu na sasa inabidi alale mwenyewe. Sababu ya umuhimu wa hatua hii ni vyema zoezi hili likafanyika kwa utaratibu bila presha yoyote wala hali ya kulazimisha.

i. Anza kwa kuongea naye muda kidogo kabla ya siku ambayo umepanga kumhamishia kwake na kumueleza kuwa ameshakuwa mtoto mkubwa na ataanza kulala mwenyewe kwenye kitanda chake. Kuanzia unapomnunulia kitanda, godoro na mashuka uwe unamueleza kuwa umenunua nini kwa ajili yake na kumuonyesha, hii itamjengea kutamani kuvitumia na kuisubiria siku ya kuvitumia kwa hamu.

ii. Tafuta mashuka yenye picha na katuni anazozipenda ili aweze kuvutika kwenda kulala. Mashuka yenye rangi moja sio mazuri sana kwa mtoto maana watoto hupendelea rangi rangi na michoro mbali mbali.

iii. Anza taratibu ili mtoto asijejisikia kuwa amefukuzwa kitandani mwako kwa kuanza kumlaza kitandani kwake wakati wa mchana na usiku awe analala kwako. Ongea naye kwa upendo juu ya kulala kitandani kwake usiku kama anavyolala mchana.

iv. Tafuta taa yenye mwanga mdogo ambayo itakuwa inawaka chumbani kwake kama anaogopa giza. Mlaze na kaa naye hadi alale usingizi. Usisahau kuomba naye na kumhakikishia kuwa Yesu yupo naye muda wote na wewe upo karibu kumsikiliza kama atahitaji chochote.

v. Usiweke mablanketi mazito kitandani kwake na kama ni maeneo ya baridi mvalishe shweta, suruali na sox maana kuna uwezekano blanketi analolitumia kusogea pembeni wakati akiwa anageuka geuka kitandani.

vi. Kuna uwezekano mtoto wako akashituka usiku na kupiga kelele au kuja chumbani kwako, ni jambo la kawaida usimkaripie wala kumlazimisha kurudi chumbani kwake mwenyewe. Nenda naye chumbani kwake na kaa naye ukimhakikishia usalama wake na omba naye kisha msubiri hadi alale tena ndipo uondoke. Kama hataki kulala mwenyewe usiku huo jaribu kumuelewa, uwe mvumilivu na kwa wakati atazoea na hatasumbua tena.

vii. Usitumie mbinu ya kusubiri kwanza alale kitandani kwako ndipo umhamishie kitandani kwake, labda kama mmekubaliana hivyo maana kama sivyo ataona kama kulala mwenyewe ni kitu kibaya ndio maana unampeleka bila yeye kujua.

viii. Ni vyema kukawa na mtu mwingine anayelala kitanda kingine pembeni na mtoto wako ili kumfanya ajisikie salama zaidi na sijione kama ametelekezwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu