Tanzania imeungana na mataifa mengine katika maadhimisho ya wiki ya ugonjwa wa shinikizo la macho duniani huku takwimu zikionesha asilimia 90 ya watu wenye ugonjwa huo nchini hawajagundulika.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma yakiwa yamebaba kauli mbiu ya dunia niangavu tunza uoni wako ambapo, mganga mkuu wa serikali Dk Aifelo Sichalwe, ametoa tamko la serikali kwa niaba ya waziri wa afya na kueleza ukubwa wa ugonjwa huo nchini.
