Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu nchini shivyawata, limewataka wazazi na walezi kutowaficha majumbani watoto wenye ulemavu.
Badala yake shirikisho hilo limewataka wawapeleke shule wapate elimu, kwani elimu ni haki yao kama watoto wengine wasiokuwa na ulemavu.
Antenna imemnasa Bi Ummy Nderiananga mwenyekiti wa shirikisho hilo, akitoa wito huo kwa watanzania.
