Maelfu ya wafuasi wa upinzani nchini Uhispania jana wameandamana mjini Madrid kumshinikiza waziri mkuu Pedro Sanchez ajiuzulu. Wengi wamekasirishwa na kitendo cha serikali yake kujadiliana na kundi la wanaotaka kujitenga la mkoa wa Catalonia, na kutaka kufanyike uchaguzi mpya. Takribani waandamanaji 45,000 walijitokeza katika maandamano ya jana, yaliyoandaliwa na chama cha upinzani cha kihafidhina Popular Party PP pamoja na kile cha mrengo wa kulia wa wastani. Kiongozi wa chama cha PP Pablo Casado aliwaeleza waandishi wa habari kuwa muda wa serikali ya Sanchez umemalizika kuanzia mwezi wa Machi. Chama chake kinapinga vikali uamuzi wa waziri huyo mkuu kushughulikia mvutano wa kisiasa na jimbo la kaskazini mashariki la Catalonia kwa kufanya majadiliano na wale wanaotaka kujitenga.