MAJALIWA : SIO UTARATBU ASKARI KUMKIMBIZA BODABODA

In Kitaifa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sio utaratibu kwa askari polisi wa usalama kumkimbiza mwendesha pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’ anapofanya makosa na kwamba kuna utaratibu wa kuwawajibisha wanapovunja sheria za barabarani.

Majaliwa ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Sylvia Sigula ambalo lilihoji juu ya mkakati wa Serikali katika kupunguza ajali zinazotokana na polisi kuwakimbiza madereva wa bodaboda. Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema hakuna utaratibu wa kuwakimbiza madereva bodaboda lakini sheria imeweka utaratibu wa ukaguzi pamoja na kuwaelimisha watumiaji wa vyombo vya moto.

“Serikali imeweka utaratibu mzuri, wakurugenzi wa halmashauri wamepewa maelekezo ya kuwapa elimu, kuwatengea maeneo katika maeneo yao. Hilo linafanyika katika maeneo mbalimbali,” amesema Majaliwa. Amewataka madereva wote wa vyombo vya moto na jeshi la polisi kufuata sheria katika usimamizi ili kuepusha ajali zinazoweza kutokea hasa pale polisi wanapowafukuza waendesha bodaboda

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu