Rob Kardashian ni Muigizaji wa Reality show ya Keeping up with the Kardashian, ni Model na anamtoto na Blac Chyna ambae pia ni baby mama wa Rapa Tyga ……
Mama wa Blac Chyna aitwaye Tokyo amesema kuwa bora mjukuu wake Dream aende kuishi na baba yake ambae ni Rob Kardashian nahii ni baada ya tabia za mama wa mtoto huyo Blac Chyna kutoeleweka.
Tokyo ameeleza kuwa Maisha ya Chyna kwa sasa yamevurugika hivyo mpaka yawe sawa anaomba Dream akaishi na Rob Kardashian.
Chyna majuzi alijikuta kwenye sakata lililopelekea polisi kwenda nyumbani kwake baada ya aliekuwa mpenzi wake wa muda mfupi Rapa Kid Buu kumshambulia Chyna ambapo mama wa Chyna amedai anawasi wasi na doc za rapa huyo.
Amesema “It doesn’t take a rocket scientist to see something is terribly wrong.” Akimaanisha haichukui mwanasayansi wa roketi pekee kuona kitu kiko vibaya sana .



