Marekani imemuwekea vikwazo mkuu wa wafanyikazi wa jeshi la Eritrea Filipos Woldeyohannes kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu katika jimbo la Tigray.Vikwazo hivyo vya Marekani dhidi ya Jenerali Filipos Woldeyohannes vinafuatia ripoti kuwa Eritrea imepeleka wanajeshi zaidi katika jimbo la Tigray linaloshuhudia mapigano.Marekani imesema itazizuia mali zote za Filipo na kwamba raia wa Marekani watazuiliwa kufanya biashara ya aina yoyote na mkuu huyo wa wafanyikazi wa jeshi la Eritrea.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema katika taarifa kuwa chini ya usimamizi wa Woldeyohannes wanajeshi wa Eritrea walihusika na ubakaji, uporaji, na unyanyasaji wa kijinsia.Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa watu milioni 4 katika jimbo la Tigray na mikoa jirani wanakabiliwa na baa la njaa.



