Kiongozi wa chama cha Conservative Boris Johnson amewashukuru wapiga kura wa Uingereza kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Disemba.
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama chake kushinda zaidi ya viti 326, Boris Jonhson amesema kwamba hatua hiyo inaipatia serikali mpya fursa ya kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya raia wa Uingereza ili kuliimarisha taifa hilo.
Chama cha Boris Johsnon kilihitaji kujipatia viti 326 ili kutangazwa kuwa mshindi lakini kufikia sasa kimepitisha idadi hiyo na kufikia viti 364.
Waziri huyo mkuu amesema kwamba uamuzi huo unampatia jukumu la kufanikisha Brexit na kuiondoa Uingereza katika muungano wa Ulaya.
”Zaidi ya yote nataka kuwashukuru watu wa taifa hili kwa kujitokeza kupiga kura ya Disemba ambayo imebadilika na kuwa ya kihistoria, ambayo inatupatia sisi kama serikali mpya fursa ya kuheshimu uamuzi wa kidemokarsia wa raia wa kulibadilisha taifa hili na kuonyesha uwezo wa raia wa taifa hili”.



