Waziri wa Madini, Antony Mavunde ametoa maagizo mbalimbali ikiwemo kuwataka Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa nchini kumpa taarifa ya orodha ya Leseni kubwa za utafiti ambazo hazifanyiwi kazi ndani ya siku saba na kuahidi kuzifuta zitakazobainika.
MAVUNDE ametoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati ufunguzi wa kikao cha Menejimenti cha Tume ya Madini kilichowakutanisha Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, kilicholenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka, pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika Sekta ya Madini.
Hatua hiyo ya Waziri inakuja kutokana baadhi watu kumiliki leseni za uchimbaji bila kuzifanyia kazi jambo ambalo linaisababishia serikali hasara.
Pia ,amemtaka Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini kuhakikisha kuwa kabla ya Juni 30, 2026, mfumo wa e-leseni unaowezesha wateja kupata huduma bila kufika ofisini unaanza kufanya kazi kikamilifu, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kupunguza urasimu katika utoaji wa huduma.
MAVUNDE, mewaagiza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuwasilisha kabla ya Februari 28, 2026, taarifa ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wanawake na vijana kupitia Mradi wa Mining for a Brighter Tomorrow (MBT).
Amewataka Maofisa hao wa Madini kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya Maofisa wa chini ambao wamekuwa wakichafua Ofisi zao na kusababisha migogoro kutokana na kujimilikisha Leseni za uchimbaji kwenye maeneo ambayo tayari yana wachimbaji.
Naye , Naibu Waziri wa Madini, Dkt. STEVEN KIRUSWA,, amempongeza Waziri MAVUNDE kwa kuendelea kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa Wizara na taasisi zake zitaendelea kushirikiana kwa karibu ili Sekta ya Madini izidi kuimarika.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, MSAFIRI MBIBO na , Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. JANET LEKASHINGOa, wameishukuru Serikali kwa maelekezo na maboresho yanayoendelea kufanywa katika utoaji wa huduma na upatikanaji wa vitendea kazi ndani ya Tume ya Madini
Katika kikao hicho Waziri Mavunde amekabidhi Magari 23 kwa Maofisa Madini Wakazi wa Mikoa ambayo yatawasaidia katika kuboresha utendaji wa kazi zao.



