Mawaziri wa Afya nchi za jumuiya ya SADC wameshauri
kusitisha kwa muda mikutano na vikao vya mawziri kutokana na
tishio la kusambaa kwa ugonjwa wa Corona katika jumuiya
hiyo.
Hayo yameelezwa na waziri wa Afya wa Tanzania Bi Ummy
Mwalimu alipokuwa akitoa maelezo kwa wanahabri juu ya yale
waliyokubaliana katika kukabiliana na virusi vya Corona.



