Tamasha lililo kutanisha watu mbali mbali katika viwanja vya mazingira bora Karatu mabapo kulitawala michezo mbali mbali pamoja na burudani ambalo, Tamasha liliandaliwa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha Mhe.CECILIA DANIEL PARESSO.
Tamasha hilo lilokuwa na lengo la kuwatanisha vijana na wazee pamoja na viongozi mbali mbali ilikuweza kuibua michezo mbali mbali ambayo imesahulika katika maeneo mbali mbali nchini.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikua ni Mwenyekiti halmashauri ya karatu MHE. JUBLET MNYENYE amesema kuwa anaomba serikali ishirikiane na wadau mbali mbali amabao wanahamasisha michezo katika jamii.
Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo mwenyeji na mbunge wa mkoa wa rusha viti maalumu amesema kuwa tamasha hilo linalenga kuinua vipaji mbali mbali ilikuweza kujitoa katika makundi mabaya katika jamii.
Aidha katika tamasha hilo limewaunganisha wananchama mbali mbali wa ccm pamoja na chadema kwa pamoja wamesema kuwa katika jamabo ambalo linaleta maendeleo katika jamii halina chama wala dini hivyo linapaswa kuungwa mkono na watu pamoja serikali.
Wakwanza kushoto ni MWenyekiti wa halmashauri ya Karatu Mhe.Mnyenye katikati ni Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Karatu na Kulia ni Mbunge wa vitimaalum Mkoa wa Arusha.
