Kikao cha 5 cha Bunge kimeendelea leo Bungeni jijini Dodoma,
huku wabunge wakiuuliza maswali na kujibiwa na Serikali.
Wabunge wameenelea kuchangia juu ya hotuba ya Waziri mkuu
na mbunge wa Viti maalum Halima Mdee alisimama kuchangia
katika sekta ya usafirishaji na kueleza shirika la ndege ATCL,
bado linaendeshwa kwa hasara kwani lina madeni makubwa.
Baada ya mchango huo wa Halima Mdee ndipo akasimama
wazuiri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba na kueleza kuwa,
madeni yanayozungumzwa na Halima made yalishalipwa.



