Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii SSRA, imesema mifuko ya na NSSF iko katika hatua za mwisho za kujenga mifumo ya ndani ya ulipaji wa fao la upotevu wa ajira, maarufu Fao la Kujitoa.
Vilevile imesema Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF, utaanza kupokea maombi ya fao la upotevu wa ajira kuanzia Novemba Mosi mwaka huu, likiwalenga waliopoteza ajira baada ya sheria kuanza kazi Agosti Mosi mwaka huu.
Kwa mujibu wa sheria mpya ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, kutakuwa na mifuko miwili nchini ambayo ni PSSSF inayohudumiwa watumishi wa umma ambayo ni muunganiko wa mifuko ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
Pia kuna mfuko wa NSSF ambao unahudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Hayo yalisema na Meneja Mawasiliano wa SSRA Sara Kibonde, alipozungumza na waandishi wa habari waliotaka kujua kama mifuko hiyo imeshaanza kutoa fao la upotevu wa ajira, ambalo
limetajwa katika sheria mpya ya mfuko wa hifadhi ya jamii.



