Seneta wa Colombia, Miguel Uribe, ambaye alikuwa amelazwa hospitalini tangu alipopigwa risasi kichwani mnamo Juni mwaka huu wakati wa hafla ya kampeni, amefariki dunia, familia yake imethibitisha Jumatatu.
Uribe, mwenye umri wa miaka 39, alikuwa Mgombea Urais kutoka upinzani wa mrengo wa kulia. Alipigwa risasi tarehe 7 Juni mjini Bogotá wakati wa maandamano ya kisiasa.
Kupitia ujumbe aliouandika kwenye mitandao ya kijamii, mke wake, Maria Claudia Tarazona, alieleza huzuni yake akisema: “Naomba Mungu anionyeshe njia ya kujifunza kuishi bila wewe. Pumzika kwa amani, mpenzi wa maisha yangu nitawalea watoto wetu.”



