Mgonjwa wa kwanza apatikana Sudan Kusini.

In Kimataifa

Sudan Kusini imeripoti kisa chake cha kwanza cha virusi vya Corona. Nchi hiyo ni moja ya nchi za mwisho za Afrika kuthibitisha uwepo wa ugonjwa wa COVID 19 ndani ya mipaka yake. Akizungumza na waandishi habari mjini Juba makamu wa rais Riek Machar amesema mtu wa kwanza alieambukizwa virusi hivyo ni mwanamke aliye na miaka 29 aliyeingia Sudan Kusini akitokea Uholanzi kupitia Ethiopia tarehe 28 Februari. Bado uraia wake haujatajwa. Taarifa kutoka kikosi cha amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS zinasema mwanamke huyo ni mtumishi wake. Machar amesema Wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la afya duniani WHO pamoja na shirika la kudhibiti magonjwa ya kuambukiza wanawafuatilia wote waliokaribiana na mwanamke huyo. Sudan Kusini tayari imefunga migawaha, vilabu vya usiku na maduka isipokuwa yale yanayouza vyakula na kuwahimiza watu kuzingatia kanuni za kujitenga.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu