Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alhaj Abubakar Kunenge ,amekagua
Maendeleo ya Mradi Sukari (Kilimo cha Muwa na Kiwanda cha
Sukari CAKaha Lake Agro Investment Ltd) kilichopo Utete
Wilayani Rufiji ,unaotarajia kuzalisha Tani100,000 za sukari
kuondoa Nakisi ya sukari kwa nchi na nyingine kuuza nje ya
Nchi.
Akizungumza akiwa Eneo la Mradi Kunenge ameeleza
wawekezaji hao wapo kwenye matayarisho ya Uwekezaji na
kuwa Eneo hilo lina ukubwa wa Hekta 15 ambalo lote litakuwa
kwa ajili ya Kilimo cha miwa .
Amesema wawekezaji hao tayari wamejenga njia ya umeme
iliyogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 100 na Barabara
inajengwa na Matarajio ya Mkoa na Serikali kwa Mradi huo ni
kupata Kodi,na Ajira ya watu zaidi 18,000.
Naye Mwakilishi wa Kampuni ya Lake Agro Investment
Abubakar Nassor amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan
kwa Mazingira mazuri ya Uwekezaji na Ushirikiano wanaoupata
kutoka Uongozi wa Mkoa.
Ametoa Wito kwa Wananchi kuchangamkia Fursa hiyo kwa
Kushiriki kwenye uchumi huo kwa kulima Miwa kwa wale
wakulima wa Nje (Out growers) Wafanyabiashara kuleta
huduma na kujipatia kipato.



