Ulinzi wa Mkuu wa zamani CIA waondolewa.

In Kimataifa

Rais Donald Trump ameagiza kuondolewa ulinzi wa aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA John Brennan,akidai kwamba ni mtu asiyetabirika katika uadilifu na asiyefuata misingi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Brennan amesema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa jitihada za Rais Trump kudidimiza uhuru wa kujieleza na kuwandama wakosoaji wa utawala wake.

Amesisitiza kuwa hili jambo linalopaswa kutiliwa mashaka na raia wote wa Marekani kuhusiana na mwenendo huu wa rais,na kuwatahadharisha pia wataalamu na wana usalama kuwa makini na hatua hizi za Trump

Brennan mapema alikaririwa akikosoa mkutano wa Trump wa mwezi July na rais wa Urusi Vladimir Putin in Helsinki uliofanyika mjini Helsinki kwamba hakuwa na maana yoyote.

Mwakajana Bw Brennan alisifu uchunguzi wa ushiriki wa Urusi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 kwamba ulikuwa umepangiliwa vizuri.

Hata hivyo Trump kwa upande amekuwa akipuuza madai hayo na kusema kuwa ni jambo linalozushwa tu kwa maslahi ya kisiasa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu